Pages

Ijumaa, 26 Septemba 2014

TIBA YA M`BA



UGONJWA WA M`BA NA MATIBABU YAKE


 M`BA ni ugonjwa wa ngozi ambao hushambulia sehemu ya kichwa, Hii hutokana na kuwepo kwa bacteria na fangasi katika ngozi ambapo hupelekea ngozi kuwasha na kuwa kavu. HUU ugonjwa hukumba watu warika zote na huonyesha makali saana wakati wa baridi na mvua.

SABABU YA TATIZO

Kitaalamu haijajulikana mpaka sasa nini huleta M`ba kichwani ila kwa tahadhari ni vyema kukausha maji pindi yanapo kua kichwani kutokana na kuoga au mvua usiache maji yakaukie kichwani na pia epuka vumbi jingi kwa kuosha vumbi pindi linapo fika kwa wingi kichwani.

MATIBABU

MAFUTA YA ZAITUNI > Chukua mafuta ya Zaituni chemsha yapate joto kisha pakaa kichwani kwa kusugulia kichwani kisha utafunika kichwa kwa muda wa lisaa limoja baada ya hapo utachukua brashi kutoa m`ba na utaosha kichwa kwa maji ya baridi.USISAHAU KUKAUSHA KICHWA 

LIMAO > Chukua vijiko viwili vya juice ya limao utasugulia kichwani na kusubiria kwa dakika 3. utachukua kikombe kidogo chenye maji na utaweka juice ya limao kijiko kimoja utaoshea kichwa mchanganyiko ho na kukausha kichwa na taulo safi utafanya hili zoez kila siku mpaka m`ba ziishe


VITUNGUU SWAUMU > Menya vitunguu swaumu kisha saga vitunguu swaumu, kisha weka msago huo kichwan kwa muda wa nusu saa kisha utatoa na kuosha kichwa kwa maji ya barid na ukumbuke kukausha maji.
DAWA hii kwa MTOTO NA MWENYE ALLERGI  itabidi uwekee maji kidogo kuepusha maumivu makali kwa ukali wa dawa




Maoni 2 :