Pages

Jumatatu, 11 Mei 2015

KITUNGUU SWAUMU



Kitunguu swaumu hakikosekani katika kila jiko duniani.Ni mmea maarufu sana kwa tiba.
Kitunguu swaumu ni jamii ya yungiyungi.
Kitunguu swaumu kilicho bora zaidi duniani ni kinachotoka MISRI kwasababu ya tabia ya ardhi yake na mto nail.
 © tibazakissuna.blogspot.com
Kitunguu swaumu kina harufu ya kipekee isiyowapendeza watu wengi ingawa kimebeba siri nyingi za tiba.Kwa ajili hiyo maana yake kilatini ni HARUFU ICHOMAYO.

 Ili kuepukana na harufu ya kitunguu swaumu baada ya kukila,kula tofaa au tafuna majani mabichi ya naanaa,au kunywa maji yaliyotokosewa karafuu.

Kitunguu swaumu kitapoteza nguvu ya tiba iwapo kitapikwa na kila kinapowekwa muda mrefu ndipo nguvu zake huongezeka (baada ya majani yake kukauka kabisa). Kitunguu swaumu kimekusanya protin 49%,sulphur 25%,kiasi fulani cha chumvi,homoni zitoazo nguvu za kiume,viuaji sumu,vikojozavyo,vitoavyo safura,vinavyoteremsha hedhi,vimeng'enyo vyenye kuyeyusha mafuta na viini vyenye kuua minyoo.Kila utafiti unapoendelea ndipo faida na maajabu ya kitunguu swaumu yanapoongezeka. 

BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU SWAUMU; 

© tibazakissuna.blogspot.com

1.Kiua sumu 

2.Kisafisha tumbo

 3.Kiyeyusha mafuta(cholestro)

 4.Huzuia mvilio wa damu 

5.Kusafisha njia ya mkojo 

6.Kutibu amoeba

 7.Kuzuia kuhara damu(Dysentery)

 8.Tumbo kushindwa kumeng'enya(Indigestion)

 9.Gesi 

10.Msokoto wa tumbo 

11.Typhoid 

12.Kidonda kilichooza 

13.Dondakoo 

14.Mabaka 

15.Baridi yabisi(Rheumatisim) 

16.Mishipa 

17.Uziwi 

18.Virusi vya homa ya mafua(Influenza) 

© tibazakissuna.blogspot.com

19.Mafua 

20.Saratani(Cancer) 

21.Kifaduro 

22.Kifua kikuu cha mapafu 

23.Kipindupindu 

24.Kutoa minyoo 

25.Upele 

26.Kuvunjavunja mawe katika figo 

27.Mba kichwani 

28.Kuupa nguvu ubongo 

29.Kuupa nguvu fizi 

© tibazakissuna.blogspot.com

30.Kuzuia meno kung'ooka 

31.Nguvu za kiume 

32.Maumivu ya kichwa 

33.Kizunguzungu/kisunzi 

34.Kutuliza maumivu ya meno 

35.Kujenga misuli na kutia nguvu 

36.Mkakamo wa ateri(Arteriosclerosis) 

37.Shinikizo la damu 

38.Kinga ya tauni na ukimwi 

39.Magonjwa ya macho 

MATUMIZI NA MAANDALIZI KATIKA KUTIBU

© tibazakissuna.blogspot.com


 Matumizi na maandalizi ya kitunguu swaumu katika tiba yanategemea aina ya maradhi unayotaka kuyatibu,hivyo basi ni muhimu kuwasiliana na wataalamu wa tiba mbadala ili uweze kupata maelekezo sahihi ya namna ya kuandaa kulingana na ugonjwa unaokusumbua.Kumbuka kama tulivyosema awali kuwa kitunguu swaumu kikipikwa kinapoteza nguvu ya tiba kutegemeana na tiba unayokusudia. 

© tibazakissuna.blogspot.com

Kumbuka pia kwamba kitunguu swaumu huweza kuchanganywa na vitu vingine mfano;maziwa,asali,habatsouda,juisi,shayiri n.k.kutegemea na maradhi unayotaka kuyatibu na kwa ushauri/maelekezo ya daktari.

© tibazakissuna.blogspot.com

Maoni 1 :

  1. kutana na mtaalamu wa mitishamba anatibu magonjwa ya ini HEPATIS B ,,MAGONJWA YA FIGO,,UTI SUGU,,NGUVU ZA KIUME,,KUKUZA NA KUREFUSHA UUME,,,KUONGEZA HIPS NA MAKALIO NA SHAPE KWA DAWA ZA ASILI NA MITISHAMAA.....KUTANA NA DR KANYAS WA TIBA MBADALA 0744903557 TANGA

    JibuFuta