Alhamisi, 18 Desemba 2014

MAJINI NI KINA NANI???

JUA KUHUSU MAJINI (WHO ARE SPIRIT/DJINN)

MAJINI na viumbe katika viumbe vya ALLAH na wameletwa duniani ili wamuabudu aliye waumba
51:56 qur aan
lakini viumbe hawa Majini wamekuwa wakisumbua sana binadamu na kuwatia maradhi ya kila aina, kwa nini majini wawatie maradhi na kusumbua wanadamu?
kuna tofauti baina ya mwanadam na jini katika maumbile yao. suurat Rahman,
majini wameumbwa kwa UPEPO WA MOTO na wanaadamu tumeumbwa kutokana na UDONGO.
lakini majini hawatupendi sana binadamu japo kuwa sote tumeumbwa na Allah.

       NINI MAANA YA JINI??

© tibazakissuna.blogspot.com
jini ni kiumbe ambaye amefichwa kuonekana kwa macho ya kibinaadamu, na ndiyo maana wakaitwa majini kwa sababu ya kuto onekana na macho ya binaadamu.
na majini waliomba kwa Allah mambo matatu baada ya kufa nabii Suleyman bin Daud as.
walichoomba

1) waishi umri mrefu

2) wawe wanabadilika kuwa kiumbe watakacho

3) wasionekane na binaadamu,

 Allah kawakubalia kwa kuwapa umri mrefu na wanaishi mpaka miaka 1000.
kisha wanabadilika kuwa kiumbe kungine lakini wanakaa kwa MUDA si umbo la kudumu, wakiamua kubadilika wanabadilika kuwa

1) paka

2) nyoka

3) binaadamu nk

na kuhusu kutoonekana wana jificha kwa wasio na elimu lakini kwa wenye elimu hawajifichi na wanaonekana, ila si kwa umbo halisi.
na majini wamegawika katika makundi 660.
pia majini wapo dini na imani tofauti               
tibazakissuna.blogspot.com 

0 maoni:

Chapisha Maoni