Ijumaa, 19 Juni 2015

FUNGA




FAIDA ZA FUNGA 

MTUME MUHHAMADI  rehema na amani ziwe juu yake amesema :: FUNGENI MPATE AFYA

pindi unapo kula chakula mfumo wa mmengenyo wa chakula huvunja vunja CARBOHYDRATE  kuwa katika GLUCOSE(sukari) kwa ajili ya kuupa nguvu mwili hivyo glucose hufyonzwa kutoka katika njia za mmengenyo na kupelekwa katika damu kisha huenda mpaka kwenye cell hapo INSULINI sasa hufungua SELLI za mwili kuingiza sukari hitajika

sasa usipo kula mwili hupungukiwa na glucose katika damu na hapo huanza kutafuta stoo (store) ya mwili inayo itwa GLYCOGEN na gylcogen inapo ishiwa basi huchoma mafuta na misuli iliyo ongezeka ili kuupa mwili nguvu.
  kwa hiyo kutokana na hayo maelezo hapo juu utajua zaid faida ya kufunga kama ifaatavyo

© tibazakissuna.blogspot.com

1) HUTIBU MARADHI YA MOYO
mafuta hua ni sababu nzur ya moyo kuto kusukuma damu ipasavyo na kuufanya moyo kufanya kaz mara mbili zaidi ili kusukuma damu ifike shemu husika sasa unapo funga na ukawa unajishughulisha na kaz za kawaida lazima mafuta hayo yaondoke mwili

2) HUPUNGUZA UZITO 

 Kwa watu walio wanene na wenye vitambi hii ina maana kua GLYCOGEN (stoo ya chakula katika  mwili ) ni kubwa hivyo unapo funga glycogen zenu zitatumika ipasavyo na kufanya mwili kupungua na kukusaidia kupandisha kinga asili ya mwili kwan acid inatoka

3) HUTIBU KISUKARI TYPE 2

katika ugonjwa huu selli za mwilim hua sio sikivu kwa insulini (kidhibiti cha glucose katika damu)  hivyo mtu akifunga insulini hua na nguvu (sensitive) ya kutuma signal  kuiambia (GLUCOSE KISAFIRISHI) kusafirisha glucose katika seli  kwani ugonjwa huu hutokea pale SIGNAL hiyo inapo zuiwa na kusababisha selli kuto chukua sukari hiyo hivyo hulepelekea sukar kuwa juu

4) HUTIBU KIHARUSI NA MISTUKO

Unapo funga mfumo wako wa moyo na mishipa (cardiovascular) hufanya kazi vyema na kutibia magonjwa yalio katika mfumo huo sasa kama tunavyojua kama  mfumo wako wa damu utafanya kazi vyema inamaana uwezo wa ubongo kupata oxygen ya kutosha utakuepo hivyo ubongo utafanya kazi ipasavyo

5) HUPUMZISHA MMENGENYO

Maradhi mengi hukulia na kukomaa katika mfumo wa mmengenyo na kisha husambaa kwenye damu pindi mmengenyo unapo kua umepumzika hali ya vijidudu vinavyo leta maradhi hufaa na mwili kujisafisha kupitia metabolism

6) HUONGEZA UMRI

ni kweli kua kula bila kushibisha tumbo hukuongezea umri wa afya njema katika maisha hivyo ubora wa kufunga ni mara mbili yake kwan maradhi meng yanatokana na kula ovyo ambapo hufanya asid kua juu na magonjwa hatar kama microbes kustawi

7) HUKUZA UWEZO WA UBONGO (akili)

kufunga imethibitishwa kuongeza uwezo wa ubongo kwani husaidia kuzalishwa kwa protein inayoitwa ( brain-derived neurotrophic factor (BDNF.)} kutoka 50 mpaka 400 ambayo husaidia kulinda ubongo kutokana na mabadiliko na pia kuzalisha neurons

© tibazakissuna.blogspot.com

 8) HUTIBU NGOZI NA CHUNUSI

kwakua mwili unapata pumziko la kusaga na kusambaza chakula basi huamishia nguvu zake katika kujenga mwili na kuuboresha haswa kuanzia kwenye ngozi 

9) HUKUTIBUA ASTHMA NA MATATIZO YA USINGIZI

funga huweza kuonda tatizo hili kwa kupunguza chumvi na maji mwilini na pia hupunguza uvimbe wa tissue hali inayo weza msaidia mtu kulala vyema na kuondosha shida ya kupumua

10) HUTIBU NAFSI

#TABIA huanza kama uamuzi kisha hua Tabia ambapo hukua na kua mraibu/teja (addicted)  na utajua kua upo addicted pindi unapo taka kuliacha jambo hilo na kushindwa hapo jua upo katika hali ya addiction
Allah mjuzi zaidi ila ili kuibadilisha tabia ya mtu huchukua masiku 30

hivyo REHAB ( sehemu za kurekebisha tabia ) hua ni siku 30 na WAISLAM tunafunga siku 29 mpaka 30
hivyo miongoni mwetu tuna ingia kufunga ili kutibu maradhi yaliyo ingia katika nafsi mfano 

KUVUTA SIGARA BANGI NA UNYWAJI POMBE

KUJICHUA > njia hii hua ni njia bora zaid ya kujikinga kwani mfumo wa divide and conquer huingia vyema katika swala la funga na kukusaidia kumiliki matamanio yako na kujihifadhi

UZINIFU >  mwenzi huu ni mwenz wa kujihifadhi kwanzia macho mpaka utendaji na ukifunga matamanio hupungua kwa kiasi kikubwa wanasayansi wamethibitisha hili kua njia nyepes na yenye kusaidia bila madhara

KUTOKUSWALI wengi wetu tumekua tukikwepa kuswali ila mara nying ndan ya mwenz huu weng wetu tunajitahid kuswali sio jambo linalo pendeza kuwasema watu wanajitahid kurud kuswal au kuwakatisha tamaa kua wanaswal kipind flan mpaka kipind flan kikubwa tupeane moyo ili kumsaidia mtu huyu swala imuingie katika tabia yake na iwe ni sehemu ya maisha yake ya kila siku kwan FUNGA ni sehemu ya kurekebisha na kumpa mtu afya ya nafsi na mwili

KUSENGENYA NA KUTUKANA > mwenzi huu hukupa haya na aibu ya kufikiria mara mbili jambo kabla hujaliendea jambo hivyo hukufunza aibu ukiwa na AIBU UNAKUA NA ADABU


HIVYO KUA MKWELI KWA SWAUMU YAKO ISHIKE NAFSI YAKO NA UTAPONA KWA UWEZO WA ALLAH MARADHI YA NAFSI NDANI YA MASIKU 29 MPAKA 30

© tibazakissuna.blogspot.com

0 maoni:

Chapisha Maoni