Ijumaa, 26 Juni 2015

FAIDA ZA TENDE



FAIDA ZA TENDE NA MAJI WAKATI WA KUFUNGUA

 TENDE imesifiwa saana na mjuzi wa  elimu kua ni tunda miongoni mwa matunda bora na hakika alisemalo MTUME MUHHAMAD REHEMA NA AMAN ZIWE JUU YAKE ni vyema kuliangalia mara mbili kwan asemalo kwa kukataza au kutusisitizia kuliendea hua kwa mwanadamu yoyote ni bora kwake kuliko tunavyo fikiria.
© tibazakissuna.blogspot.com
VILIVYOMO NDANI YA TENDE

Energy282 Kcal
Proteins2.5 g
Fiber8 g
Fat0.4 g
Folate19 mu gs
Iron1.09 mg
Vitamin K2.7 mu g
Magnesium43 mg
Potassium656 mg
  
MARADHI YA MOYO ::
                     tende husaidia moyo na mishipa kwa kua hufyonza cholestrol katika mishipa na FIBER hujulikana kwa kusaidia moyo , Hivyo hua na msaada kwa watu wanao ugua shinikizo la damu

© tibazakissuna.blogspot.com


KUPUNGUZA UZITO ::
                    tende hua na tabia ya kushibisha upesi kutokana na wingi wa fiber ambayo huleta nguvu na mwili kuwa na maridhio ya kiwango cha chakula kilichopo tumboni

 KUSAIDIA MMENGENYO ::
        tende tunda lenye fiber nyingi ambapo husaidia mmengenyo wa chakula kwa kusafisha (gastrointestinal system) na kuupa mwili nguvu  

HUSAIDIA AFYA KWA MJAMZITO NA MWANAE  ::
kwa mjamzito kula tende kuna faida zaid ya nane kwake yeye na mwanae haswa kuimarisha afya zao na pia ni msaada mkubwa kwa mwanamke anaetaka kujufungua husaidia kujifungua bila misukosuko ya njia na uchungu

HUIMARISHA MIFUPA ::
               Tende pia hua na calcium ambayo huimarisha mifupa na kutibu maradhi ya mifupa na maumivu (arthritis)


HUIMARISHA UBONGO ::
                  Utafit ulio fanyika (JAMA INTERNAL MEDICINE) inaonyesha kua ubongo huimarika na kufanyana kufanya kazi vyema kwa akili kutokana na VITAMIN B6


HUONGEZA NGUVU ZA KIKE NA ZA KIUME ::
  Changanya tende  maziwa na asali jaribu alafu utanipa jibu lake


TIBA YA KUHARISHA ::
    hutibu kuharisha kama utachanganya na asali

HUONDOSHA MALARIA ::
    Kula chembe saba baada ya Salat alfajri pamoja na maji ya vugu vugu kikombe kimoja

MTUME MUHAMADI REHEMA NA AMANI ZIWE JUU YAKE ALIKUA AKIPENDA KULA TENDE NA KUTUHUSIA KUFUNGUA KWA TENDE 

© tibazakissuna.blogspot.com


>> KWANN UFUNGULIE MAJI YA MOTO NA SIO YA BARIDI NA SODA

a) unapo kua umefungulia maji ya moto husaidia kuyeyusha mafuta mafuta ndani ya mwili 

b) maji ya moto husaidia kuyeyusha chakula na kufanya mmengenyo ufanyike kwa wepesi na uchafu kutoka kwa wepesi

c) husaidia ngozi kupuumua kutoa jasho na kuondoa mafuta futa na kufanya upumuaji mzur na kujiskia upo vyema 

d) huondoa uteute ambapo uteute husaidia kushika wadudu na kuowaangamiza hivyo unapo kunywa maji ya moto hufungua njia ya koo na pua na kukusaidia koromea kushusha uteute utaoenda kutolewa kama uchafu

e) unapo kunywa maji ya moto mwili hupandisha joto na kukusaidia kuondoa uchafu kwa njia ya jasho

© tibazakissuna.blogspot.com

KWANIN USITUMIE MAJI YA BARIDI

1) Maji ya baridi hufanya mfumo wako wa mmengenyo kufanya kwa tabu kwani mwili utapoteza nguvu zake kuhakikisha maji yamekua ya moto nguvu hiyo huenda ingetumika katika kumengenya chakula ulicho kula

2) maji ya baridi hufanya mafuta kuganda hivyo kama ulikua na sababu ya kupungua uzito zoezi litakua gumu 

3) huatarisha kushindwa kufanya kazi kwa figo

4) soda zina madhara mengi ikiwa utaanza kufungulia soda una nafasi kubwa ya kufyonza sumu yake vyema 

© tibazakissuna.blogspot.com
 
FAIDA KWA ALIE FUNGULIA TENDE

1) tende huzuia kiungulia na pia husaidia mmengenyo wa vyakula hivyo mtu anae futuru hua ni funguo inayo saidia vyakula utavyo kula

2) tunajua tende husaidia kupunguza kasi ya kula haswa ukifungulia hua ni sababu ya kukusaidia kuto kula saana na kufanya afya yako kuzid kuimarika

3) husafisha mwili kutokana na magonjwa na kuupa mwili nguvu 
© tibazakissuna.blogspot.com

IKIWA MUDA UTAPATIKANA TUTAELEZEA FAIDA ZA TENDE KWA MAMA MJAMZITO


0 maoni:

Chapisha Maoni