Suala hili limekuwa likisemwa sana na baadhi ya watu,
haswa wale walio wavivu wa kufanya kazi na kupenda maisha ya starehe bila kutumia nguvu na akili zao.
utamsikia anasema kwamba,bora nioe jini nipate hela.
loh wewe hujui usemalo,
sababu ya kukwambia hivyo hujajua kuwa majini wana tawala na maisha yao kivyao kama ilivyo kwa binaadamu,
WAO WANA
© tibazakissuna.blogspot.com
JESHI,
ASKARI,
MADAKTARI,
MAWAZIRI,
WABUNGE na MADIWANI wao,
kuna WASELA na WAVUTA BANGI.
hivyo wao wana serikali yao na HELA ZAO.
HELA YA JINI haitumiwi na mwanadamu,
kama vile pesa ya Misri haitumiki Malawi,
wala ya Tanzania haitumiki Marekani.
na majini pesa yao haitumiki kwa wanadamu sababu serikali yao na wanadamu ni tofauti kabisa.
WALE WANAO SEMA WANAPEWA PESA NA MAJINI WANAPATA WAPI ?
pesa ile huwa majini WANAIBA katika MADUKA na BIASHARA za watu kisha unahongwa,
MAJINI wenye kufanya haya ni wale majini mahaba aina ya GHUULI, wale wenye CHUMA ULETE.
kwani majini hawa hatari ni wezi sana na ndiyo wenye mambo ya kuiba watu na kuwafanya misukule.
jambo hili halifai kabisa katika uislam 6:128-130 QUR AAN
kama ulikuwa unahongwa basi rudisha pesa ya watu,
jini hana pesa ya kukupa zaidi ya pesa ya wizi
© tibazakissuna.blogspot.com