Ijumaa, 2 Januari 2015

TIBA YA KUKUZA NYWELE



Unajua kwamba nywele ni moja kitu chenye thamani kubwa sana katika maisha?

watu hutumia pesa nyingi sana kwa ajili ya kutengeneza  nywele, kiasi kwamba wale wenye nywele vipilipili huwa katika  wakati mgumu mpaka huamua kusuka nywele za kuunga ambapo ni KINYUME  na UISLAM
lakini sababu ya yote ni nini?

Lengo anataka na yeye aonekane ni mwenye nywele ndefu.
Pia isitoshe nywele ni katika urembo wenye kuvutia sana kwa mwanamke pindi akijua kuzilinda. sasa ni vipi utakuza nywele na kuzilinda ili zisikatike?
tibazakissuna.blogspot.com   hapa unapata njia bora isiyo kupatia dhambi kwa mola wako.

1) ILI NYWELE ZIKUE

chukua vifuavyo:
chukua HULBA {uwatu} kisha chota vijiko 5 vikubwa halafu CHEMSHA kwa maji lita 2,
yakisha chemka vema, oshea nywele na baada ya kuosha  chukua kitambaa UZIFUNGE vyema kichwani kwa muda wa nusu saa, 
baada ya nusu saa fungua na uoshe kwa maji ya KAWAIDA.  
fanya kwa siku 11 basi utakuwa na nywele ndefu zenye kuvutia.

2) ILI ZISIKATIKE

Chukua HINA na SANAMAKI
, kisha chemsha pamoja halafu oshea nywele kama unavyo oshea shampoo, 
basi utaondoa mba na nywele kuto katika katika.
tibazakissuna.blogspot.com

1 maoni:

  1. Aslam Aleykum jamiya samahani naomba kuulizia jina lingine au lililozoeleka bara la maneno UWATU NA SANAMAKI wabillah tawfik

    JibuFuta