Alhamisi, 8 Juni 2017

NYOTA NA MILANGO YA MARADHI


NYOTA NA MLANGO WA MARADHI

nyota zina mgawanyo wa hali na tabia, pia huongoza maarifa ya kazi
Lakini leo tunaangalia mlango wa maradhi wa kila nyota
tibazakissuna.blogspot.com
1. Punda 

Nyota hii mwenyewe husumbuliwa na maradhi ya kichwa na moyo, kwa sababu huwa wanasumbuliwa au hurogwa kwa jini Khafqaan
Mwili huwa na joto unababua kama Moto mwilini
Tabia ya nyota ni moto
Kazi zake ni usafirishaji na utumishi ,siku ya bahati jumanne na nuks jumapili

2. Ng'ombe

Hii Nyota hufanyia kazi katika udongo, siku yake ya bahati ijumaa na nuks jumatano
Maradhi yake, viungo kulegea kama mtu aliye choka na majini kama maymuna huusumbua sana mwili huo, wanapenda mapenzi sana
kazi ni biashara ya mazao au uchimbaji madini
3. Mapacha
Inafanya kazi jumatano, na nuks jumatatu
Tabia yake upepo, kazi za mawasiliano au elimu ya anga
Biashara zote za vyombo vya mawasiliano
Maradhi
Husumbuliwa kwa marogi kupitia jini twayr, huwa wanaota kupaa, chunus sugu, na matatizo ya uzazi
tibazakissuna.blogspot.com
4. Kaa 

Ina fanya kazi jumatatu na nuks yake jumamosi
Nyota hii ni nzuri kwa utawala japo kuwa mara nyingi haipati sifa hata ikitawala vzuri, utendaji ni maji
Kazi huduma zote za jamii, utumishi na kutumika kwa maslahi machache pia hujiamini sana
Maradhi huingiwa sana na maradhi ya mapenzi kama limbwata, husda ya ndugu na marafiki kumuona kama ana nufaika hali hana maslahi zaidi ya utumishi

5. Simba

Inafanya kazi jumapili na nuks ijumaa
Maradhi yake, vidonda vya tumbo, kiungulia na kuchukiwa haswa na majirani
Hutumika sana subian kudhuru watu hawa
Kazi ni usimamizi na uangalizi wa mali, na kutunza amana za watu japo uaminifu kwao huwa mdogo,tabia moto

6. Mashuke

Hufanya kazi jumatano na nuks jumatatu
Nyota yenye asili ya kipato kwa kazi za mahesabu au uhasibu na mambo ya utunzaji amana
Hutenda kazi katika udongo
Husumbuliwa kurogwa kwa jini Ummu subian
Maradhi ya strock, ganzi na baridi kama rheumatism
Maradhi ya moyo na cholesterol tatizo la kushindwa kufanya jimai

7. Mizani

Inatenda kazi ijumaa na nuks jumatano
Husumbuliwa na husda na wivu, majini kama tawaabia, alkhannaas, zawaabil husumbua sana watu hawa.
Hawa watu ni upepo na hawana misimamo

8 Nge

Hutenda kazi jumanne na nuks jumapili
Hutenda kazi kwa maji, watu wenye jadhba na maamuzi ya kujilaumu, wana mikono ya kuharibu na kuto dumu na vitu. Wana maeneno mengi, na akili huwa vichwa vyao vipo haraka kidogo
Majini aljinnu saakiniyna au khaadimu sihr huwa athiri sana
Wengi wao husumbuliwa na chale za wanga huwa wana maradhi ya kukakamaa misuli
tibazakissuna.blogspot.com
9. Mshale 

Inatenda kazi alkhamis na nuks jumanne
Nyota ya biashara, nyota hii hata iuze matapishi itaingiza pesa
Ni nyota hatari kwa kuchezewa na washirikina, wengi wao hupatwa uchizi wa ghafla kwa kuchukuliwa nyota, ni nyota yenye uaminifu zaidi na misimamo, pia maamuzi yao ni makubaliano huwa hawaamui wenyewe kwa matakwa yao. Wavivu sana wa kula na kunywa, husumbuliwa haraka na sukari, figo na homa za matumbo

10. Kondoo (mbuzi) 

Ina tenda jumamosi na nuks alkhamis
Tabia udongo
Maradhi ya kichwa, khofu, matatizo ya viungo kulegea na kuishiwa nguvu na macho kusumbua bila sababu za kidaktary, hutokana na kusumbuliwa na husda za wachawi
Kwani kwa kazi za shamba nyota hii ina nguvu sana pia elimu ya misitu na mimea. Majini kama hamaatu nnisaai, jinnu saakiniyna na ummu subian, huwafanya wakawa na madhaifu mengi ya ndoa na uzazi

11. Ndoo 

Inafanya kazi jumamosi na nuks alkhamis
Husumbuliwa na matatizo ya akili, moyo pamoja na matatizo ya kuanguka, si ajabu kwa mtu huyo
Na ikitokea wanaishi karibu na makaburi rahisi kukumbwa na jinni mayyit
Na wazuri kwa kazi na elimu ya kuhifadhi na usindikaji, au ujasiriamali
tibazakissuna.blogspot.com
12. Samaki 

Hutenda alkhamis na nuks jumanne
Husumbuliwa na awaaridhwu, riyh riyhaan, na majini wengi sana kwa kuwataja mmoja mmoja ni ngumu
Pia huwa ni watu wenye kuandamwa na mambo ya kiasili kuanzia maradhi, afya na rizqi
Husda nyingi hufanyiwa na wanawake
Kazi ya kuhudumia jamii kama Jeshi, utabibu na sheria zinawafaa sana
Kama unaziada karibu inbox
Vigezo na mashart kuzingatiwa
tibazakissuna.blogspot.com


Baada ya kujua ulivyo ndiyo uweze kusaidika kwani wapo ambao nyota zao huahama na wengine kutembelea nyota ya washirika, ili kusaidiwa tatizo la kinyota huhitajika sana utumiaji wa Aayatu rizqiya, ayaatu l fat hi, na ayaatul khawaatimu
Swihat shifaa na zaytu shifaa ni lazima kupatikana kwa dawa za kula,kuoga na kupakaa 

6 maoni:

  1. Kutana na mtaalamu wa mitishamba toka tanga anatibu ugumba uzazi nguvu za kiume kukuza uume na kunenepesha uume kukuza hips shape na makalio kwa mvunge. Kuondoa vitambi. .kuondoa harufu mbaya na maji ukeni. .zindiko ..uchawi.na mvuto nyota mpigie dr kupitia 0744903557 tanga

    JibuFuta
  2. Naomb kuifaham Nyota yangu.

    JibuFuta
  3. Asalam aleykhum Mimi nyota yangu Ni punda Na yote uliyoipeleka ndio maradhi yangu mwilikuwaka moto kwa ndani .matatizo ya Kulikuwa Na moyo mda mwingine miguu unataka moto,kichwa kuuma n.k naomba msaaada ...nauseous vp haya matatizo Na pia nataka nyota yangu ung'arishe Kama zamani

    JibuFuta
  4. Habari? Nilitaka kuuliza kwa upande ws dawa za kunywa,kuoga ambazo zinapatikana Kweny maduka ya dawa za asili, ambaz zingesaidia luondoka na magonjwa, mabala nuks. Haswa kwa sisi wenye nyota ya Mashuke ufafanuz wako shekhe

    JibuFuta
  5. Sa mi mwenye nyota ya mbuzi nifanye nini juu ya nuks za alhamisi na iweje juu ya kujikinga na uchawi

    JibuFuta
  6. Mcheni Allah kabla hamjafa Kama Kama ingekuwa maradhi yanaangaliwa kupitia nyota basi mtume angekuwa wa kwanza kuwafundisha maswahaba

    JibuFuta