Jumatano, 27 Julai 2016

KUCHEZEWA NYOTA



NYOTA ILIYO CHEZEWA

Leo nataka kuongea kitu kitakacho kuwa kama kigeni kwa baadhi yetu, lakini ni maarufu pia kwa baadhi yetu.
Nyota ni sehemu ya mzunguko wa maisha yako mwanadamu, ambalo fungamano hili huenda kabisa na maisha ya binaadam kiutendaji kazi, rizk na maradhi.

 
Ukiongea nyota wapo watu wataona ni elimu ya ajabu ama shirk fulani, kwa sababu wengi wetu tunapenda uzungu na kuona kama elimu iliyo katika mfumo wa kiarabu imepoteza dira. Nyota zipo aina hii
كواكب،بروج،نجوم
Kawaakib,Buruuji na Nujumu. 


Ambapo kwa wasomi wa kizungu elimu hii kwao huwa ni astronomy
Ni elimu ya mambo ya geography.

hapa nyota ya maisha ya mwanadamu ni hii buruuji, ambayo hii buruji huwa ni Sayari na njia zake ni kawaakib ama obirt
 
Ambapo zipo sayari 12 na Obirt 12
Sayari hizi ni Hamal punda, Thaur ng'ombe mume, Aljauzau mapacha, surtwaan kaa, asadu simba,alqadhwyimat mashuke, mizan, aqrab nge,qaus mshale,Jady,dalwu na huut ama samaki.na kila nyota zina sifa nne ambazo Maji,Udongo,Moto Hewa
Hapa ndipo mtu anapo weza kukuchezea na kuharibu maisha yako. Audhu billaahi min dhaalik

 
© tibazakissuna.blogspot.com

 
Epukeni sana ndg zangu waganga wenye tabia za kuharibu maisha ya watu
Kwa mfano mtu ambaye nyota ya mashuke huyu nyota hufanya kazi jumatano, sifa mapato, utendaji wake udongo. 


Huyu ndiye mwenye hatari kwa mkulima na hatari kwa mfanya biashara anaweza kuchezewa nyota kwa maslahi ya muhuni mmoja anaye taka kulima au biashara na nyota yake haikubali kazi hiyo.
Hizi nyota huwa zinautendaji wa kila siku na nuksi ya kila siku kwa wiki nzima, zikiwa chini ya Malaika husika na malaika hawa wapo Saba, Ruuqayaail,Jibril,Samsamaail,Miykaail,Swarfayaail,Ainayaail na Kasfayaail hao ndiyo Malaika wa jumapili mpaka jumamosi kila Malaika na siku yake kwa nyota husika.
 

MTU ANACHEZEAJE NYOTA YAKO?? 
 
AUDHU BILLAAHI MIN DHAALIA

 
niwaombe matabibu kwa kweli suala la kucheza na nyota ya mtu ni dhambi iliyo kubwa na Muogopeni Allah

 
© tibazakissuna.blogspot.com

 
Kinacho fanyika ni kuchukua kivuli kwa siri na kuweka na madawa husika kisha kutumiwa sehemu husika, na hao watumiaji ndiyo watu ambao unaweza kukuta unatumia nyota ya ndg au mfanyakazi, na kama mfanyakazi basi huyu anaweza kutukuzwa hata kama elimu yake hairuhusu kukaa katika wadhifa huo, au atafanya kosa kubwa na kupata msamaha wa mwepesi na haraka bila Shart.kama itatumiwa na ndg hapo ndiyo majanga.
 

Dalili gani utajua iwapo nyota inatumiwa au kuchezewa???
 

Hapo aliye chezewa nyota huwa
 
1 mambo yake yanaharibika hovyo

 
2 watu hawamjali

 
3 huwa kama mwehu au zezeta fulani

 
4 watu watamtenga

 
5 pesa kutoweka mazingira ya ajabu

 
6 kufanya kazi kwa bidii na kutoona faida ya kazi

 
7 kuumwa ugonjwa wa ajabu ima kurukwa akili

 
8 mtu mzima watu kumfanya kama mdoli kwa kukosa heshima

 
9 akili inakuwa kama imefunikwa na kukosa muelekeo mpaka kutamani kujiua

 
NK

 
Ni miongoni tu mwa dalili.
Wafanyaji hayo muogopeni Mola wenu.
Pia mtendewaji unaweza kuambatana hata na tabia ya kuota utajiri hali ya kuwa hela ya kodi hujui pa kuitoa.
Unakuwa na wakati mgumu ukichezewa na ndugu, na utajiona una bahati isiyo na mafanikio ukichezewa na bosi.
Msingi kwa upande wa tiba
Upate Sheikh mjuzi wa elimu ya tiba isiyo na shirk na iwe tiba ya kisheria kisha ufanyiwe visomo vya Aayatu l fathi na Aayatu rizq

 
Huku ukiwa unapakaa zayt shifaa
tibazakissuna.blogspot.com
+255784638989
+255713826838

1 maoni:

  1. Mnazo dalili za kuran na sunnah juu ya NYOTA na ugumu wa rizq?

    JibuFuta