Jumanne, 28 Julai 2015

JINI 2



JINI NI NINI?
 
Kwanini majini wanasumbua binaadamu?

 
Majini kusumbua binaadamu in kutokana wivu ambao majini wamekuwa nao nafsini mwao kwa ajili ya wivu na uroho Wa madaraka. 


Kumbuka kuwa majini waliumbwa kabla ya binaadam na walikuwepo ardhini kabla ya mwanaadam na mwanadamu ni kiumbe Wa mwisho kuja duniani 76:1-2 Quran
 
Hivyo kuwa mwanadam kiumbe wa mwisho kuja duniani maana ni kuwa majini waliishi kabla yetu na kutawala ardhini. Lakini walimuasi Allah na kuangamizwa na kubaki wachache ambao walikimbia na kujificha kama vile


© tibazakissuna.blogspot.com 

baharini 

 
mitoni

 
visimani

 
milimani

 
Majumba mabovu

 
Chini ya miti na mitaroni nk.

 
Kwa wale walio salia ikiwamo Ibilisi mlaaniwa wao baadhi wakachukua jukumu la kuto kukubali kumheshimu mwanaadam pindi Allah alipo sema Inniy jaailun film ardh khaliyfat.

 
Ibilis alionesha ukaidi na kuanza kupinga amri ya kumheshimu mwanaadam kwa amri ya Allah alipo waambia malaaika
Sjuduu li Aadama. Fasajaduu illaa iblisa abaa wastakbara wakaana minal kaafiriyna

 
Kwanini awe miongoni mwa makafiri? Sababu yeye sio kafiri Wa kwanza ila walianza kukufuru baba zake
Alipokataa akalaaniwa na yeye kuamua kufanya juhudi ya kumpoteza mwanaadamu ili mwanaadamu aharibikiwe. 

© tibazakissuna.blogspot.com
Ndipo yeye na vizazi vyake na washirika wake wakawa na Nazi maalum kumsumbua mwanaadamu ili mwanaadamu ashindwe kumhishimu muumba na kuwatukuza majini na majini kutaka kuheshimiwa kwa majina matukufu kama kuitwa walimu au mawalii au masharifu au ruhani ima akataka aitwe Suleiman bin Daud
Audhu billaahi min dhaalika.
tibazakissuna.blogspot.com

0 maoni:

Chapisha Maoni